Ufugaji bora wa kuku

Mfugaji wa kuku ana jukumu la kuhakikisha kuku wake wanaishi katika mazingira mazuri kiasi cha kutosha kufanya uzalishaji.

Utangulizi

o  Kuku: ni jamii ya ndege wanaofugwa

o  Vifaranga: Ni watoto wa kuku waliotoka kwenye yai wenyeumri kuanzia siku ya 0 mpaka miezi 2.

o  Kuku wanaokuwa: Hawa ni kuku waliotoka kwenye hatua ya vifaranga,umri ni miezi 2.5- 5.

o  Kuku wakubwa: ni kuku waliomaliza hatua ya kuku wanaokuwa,umri wao ni kuanzia miezi 5 na kuendelea.

Faida za kufuga kuku chotara

 • Chanzocha Chakula – nyama ya kuku na mayai (protini)
 • Chanzocha kipato – mkulima hupata fedha akiuza kuku au mayai.
 • Chanzocha ajira – ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii.
 • Gharamanafuu za kuanzisha na kuendesha mradi huu.
 • Mbolea– kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao namabwawa ya samaki.
 • Kuendelezakizazi cha kuku wa asili hapa nchini.
 • Manyoyaya kuku hutumika kama mapambo, kutengenezea mito na chakula cha mifugo.
 • Shughuliza utafiti na mafunzo.

Mambo ya kuzingatia katika ufugaji wakuku chotara

Ufugaji wa kuku unahitaji mtaji kulingana namalengo yako, kuna vitu vinavyo hitajika kukamilika kabda hujaanza kujihusishana mradi huu

      Mahitaji ni yafuatayo

 • Eneona usalama
 • Bandabora
 • Ainaya Kuku (Chotara)
 • Vifaa
 • Usimamizi

Njia tofauti za kufuga kuku.

Kuku chotara anaweza kufugwa kwa mifumo ifuatayo ya ufugaji, kwaajili ya tija na udhibiti wa magonjwa:

     i.        Kufuga nusu ndani – nusu nje

Huu ni mtindo wa kufuga ambao kuku wanakuwa nabanda lililounganishwa na uzio kwa ajili ya chakula, maji na mazoezi.

     ii.        Kufuga ndani ya Banda

Njianyingine ni kuwafuga kuku ndani tu. Katika njia hii, kuku hukaa ndani wakatiwote. Njia hii ya ufugaji utumiwa zaidi na wafugaji wa kuku wa kisasa

Banda Bora la kuku

Kuku wanahitaji sehemu nzuri ya kuishi na kukua vizuri.

Sifa za banda bora la kuku.

 • Liwejengo imara.
 • Liwerahisi kufanya usafi.  
 • Eneola nje kuzunguka banda kuwe na usafi wa kudumu.
 • Liwena nafasi ya kutosha kwa kuku waliopo.
 • Liwezekuingia hewa na mwanga wa kutosha(Liwe na madirisha makubwa).
 • Lisiwena joto sana au baridi sana.

Kuku chotara

Mfano wa kuku chotara ni Sasso, Kuroiler na Chiku

Faida ya ufugaji kuku chotara

 • Hutagamayai kati ya 150 - 250 kwa mwaka.
 • Mkulimaanauwezo wa kuendeleza kiazazi chao.
 • Wastahimilivuwa magonjwa ukilinganisha na kuku wa kisasa.
 • wanaumbilekubwa na kutumika kwa nyama na mayai.

Changamoto ya kuku chotara.

Wanauwezo mdogo wa kustahimili magonjwa na wanahitajichakula kingi ukilinganisha na kuku wa kienyeji.

Lishe ya kuku chotara

Kuku chotara huitaji chakula chenyemchanganyiko wa virutubisho kwa viwango maalumu vya kuandaa chakula bora kwaukuaji na afya ya kuku virutubisho hivyo ni kama vile Wanga/nishati, Protini,Madini na Vitamini, huandaliwa kwa rika tofauti za kuku hao kuanzia vifaranga,kuku wanaokuwa na kuku wakubwa. Chakula uchukua asilimia 70% ya mtaji wakohivyo unapataka kufuga sehemu kubwa ya mtaji ni chakula.

Vifaa

Katika ufugaji wa kuku ni lazima kuwa na Vifaakwa matumizi mbalimbali ambazo ni pamoja na:

 • Vyombo vya Chakula na maji
 • Viota vya kutagia navichanja vya kupumzika na kulala
 • Matandiko (Malanda, pumba za mpunga na nyasi kavu):kuweka chini ya sakafu.
 • Kitalu/Bruda (kinahitaji chanzo cha joto na mwanga):kwaajili ya kulelea vifaranga.
 • Vifaa vya usafi: Fagio, kwanja na mabrush
 • Vifaa vya kutunzia kumbukumbu: mfano madaftari, Kompyuta au ubao

Faida za kutumia vyombo bora:

 • Huzuia kuchafuka kwa chakula.
 • Huzuia kupotea kwa chakula.
 • Hupunguza uwezekano wa kuku kuambukizwamagonjwa kama vil coccidiosis, minyoo n.k.

Wadudu na Magonjwa Ya Kuku.  

Magonjwa ya Kuku

 • Magonjwayanayotokana na Bakteria kama vile Mafuaya kuku, Taifodi ya kuku, Kuhara nyeupe, Kipindupindu cha kuku,Mycoplasmosis ya kuku.
 • Magonjwaya Virusi kama vile Mdondo/sotoka/kideri,Gumboro na Ndui
 • Magonjwaya protozoa kama vile Kuhara damu(Coccidiosis)
 • Wadudu;Viroboto, Utitili na Ukurutu
 • Magonjwaya ukosefu/Upungufu wa Lishe bora: Ukosefu/upungufu wa vitamini A, B1, B2, B7, E (kichaa cha vifaranga), D na ukosefu wamadini ya Calcium na Phosphorus n.k.

Dalili za Jumla za Magonjwa ya Kuku

 • Kuku kupoteza hamu ya kula.
 • Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu(Kutochangamka).
 • Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
 • Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. - Machokuwa na rangi nyekundu.
 • Kujikunja shingo, Kukonda na Kukohoa.
 • Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni namachoni.
 • Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani auwenye mchanganyiko na damu au cheupe.

 

Tiba nakinga za kuku

Madawa ya asiliyatokanayo na mimea yanayosaidia katika tiba na kinga za maradhi mbalimbali yakuku. Sehemu za mimea zinaweza kuwa: Majani, Magome, Mbegu, Maua au Matunda.

Umuhimu wa kutumia tiba zenye asili ya mimea:

 • Hupatikana kwa urahisi.
 • Ni rahisi kutumia.
 • Gharama nafuu.
 • Zinatibu vizuri.
 • Hazina madhara.

Mwarobaini (Majani, Mizizi, Magome): Hutibu magonjwa yafuatayo: Typhoid, Kuzuia Kideri, Kuhara, Mafua,Vidonda.

Shubiri Mwitu (Aloe vera):Inaweza kutibu Kideri au mdonde au Sotoka inyweshwe kabla ya kinga. Homa yamatumbo (Typhoid), Mafua (Coryza), Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).

Mtakalang’onyo (Euphorbia): Hutibu: Kideri – inyweshwe kabla kuzuia Gumboro, Ndui, Kuhara damu(Coccidiosis). Mbarika (Nyonyo):Hutibu Uvimbe. Weka majani ya mbarika ndani ya majani ya mgomba kisha wekandani ya jivu la moto, kisha kanda sehemu yenye uvimbe kwa kutumia majani hayoya mbarika.

Mlonge (Mlonje): Hutibu:Mafua, Kideri - inyweshwe kabla kwa kukingaKipindupindu cha kuku (FowlCholera), Homa ya matumbo.

Ndulele (Dungurusi, Makonde, Tura/Ndula): Majani hutibu Minyoo, Matunda hutibu Vidonda.

Minyaa (Cactus): Hii niaina yenye majani manene-hadi kufikia nusu nchi na mapana hadi kufikia upana waviganja viwili vya mikono. Minyaa hutibu: (Angalia inaunguza au kubabua).Vidonda. Ngozi na Uzazi.

Pilipili Kichaa:Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwamuda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhikuingia).

Kutokana nakwamba mimea dawa inayo tumika haina madhara katika mili ya ndege endapoikachanganywa zaidi ya moja na kwa kiwango na uwiano sahihi, wafugajimnashauliwa kuchanganya zaidi moja kutokana na upatikanaji wake, mfanomchangayiko wa mwarobaini, alovera, mpera, mpapai, mlongelonge, pilipili n.k.Mchanganyiko wa mimea dawa hiyo ni bora zaidi kudhibiti magonjwa mengi ya kukukwa wakati mmoja.

Usimamizi

Shamba la kuku chotara linatakiwa kuwa na mifumoya kuzingatia katika Ufugaji

Mfumo wa ulishaji chakula: Lisha kuku wako mchanganyiko wa chakula nakwakiwago kinachohitajika kwa siku. Kuku ulishwa mara mbili au zaidi kwa siku.

Mfumo wa unyweshaji maji: Kuku wanatakiwa kupewa maji salama,yakutosha na yawepo bandani muda wote.

Mfumo wa udhibiti wa magonjwa:

 • Biosecurity:Ni kuzuia magonjwayasiingie ndani ya banda la kuku na yakiingia yasitoke; ikihusisha Usafi, tengakuku wagonjwa na wa rika tofauti, kutakasa miguu kabla yakuingia bandani,kunawa mikono na usiruhusu watu kuingia hovyo kwenye banda la kuku.
 • Mfumowa utoaji Chanjo:Chanjo ni kinga anayopatiwa kuku mwenye afya ili kujikinga na magonjwa. Kukuwanatakiwa kupewa chanjo ya magonjwa korofi kwa wakati sahihi. Mfano wa chanjoni chanjo ya ugonjwa wa sotoka/Mdonde/kideri, Gumboro na Ndui.
 • Tiba: Kuku wanaoumwa watengwe na kupewa tibaipasavyo.

   

Mfumo wa Kutunza kumbukumbu

Katika shamba la kuku ni muhimu kuwa na mfumowa kutunza kumbukumbu, kumbukumbu za idadi ya kuku, Uokotaji wa mayai,Afya,kumbukumbu za chakula.