Bustani Za Jikoni

Umuhimu wa mboga katika lishe ni jambo linalofahamika kwa miaka mingi sana. Mlo hauwezi kuwa kamili bila kuwa na mbogamboga.

Nini Maana ya bustani za jikoni?

Bustani ya jikoni ni bustani ya nyumbani ambayo inaweza kuipatia familia yako mboga mboga zenye kijani kibichi kwaajili ya matumizi ya kila siku.

Faida ya bustani za Jikoni

  • Kupata mboga mboga na matunda
  • Huokoa muda na pesa kwa kutokwenda sokoni
  • Kuwa na familia yenye afya, na kupunguza gharama za matibabu kwa kutumia, mboga mboga za kilimo hai zilizozalishwa kwa mbinu salama kwa afya ya mlaji.  
Umuhimu wa mbogamboga katika lishe ni jambo linalofahamika kwa miaka mingi sana. Mlo hauwezi kuwa kamili bila kuwa na mbogamboga kwani ni ndo chanzo kikuu cha viini lishe hasa vitamini, madini, chumvi, protini na nyinginezo.

Mambo ya kuzingatia ili kuanzisha bustani za jikoni.

  1. Mpangilio wa bustani:  Ukubwa wa bustani, mwelekeo wa jua na kivuli, ukaribu wa miti na mifumo ya mizizi, mteremko, umwagiliaji.
  2. Vitalu vya bustani na maandalizi ya udongo
  3. Kukuza bustani yako: nini cha kupanda, misingi ya upandaji.
  4. Matengenezo ya bustani, uvunaji na uhifadhi
Bustani za jikoni ni njia inayo changia usalama wa chakula na masuala yanayohusiana na afya. Kwa kula matunda na mbogamboga zilizopandwa karibu na nyumba zetu, tunakuza hali ya afya na kupunguza gharama za uzalishaji.

Vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya bustani ya jikoni

  1. Trowel (Mwiko): Hutumika kupasua mashada ya udongo, kuchimba mashimo madogo, Kupandikiza miche na hata kuchimba magugu.
  2. Mkasi wa Kupogoa au kupunguzia: Hutumika kuvuna mazao mapya au kukata vichaka vya beri
  3. Keni ya umwagiliaji: Tumia kwa kumwagilia mimea na maji mapema asubuhi wakati halijoto ni ya baridi. Epuka kumwagilia mchana, ambayo itayeyuka haraka sana.
  4. Bustani reki: Hutumika kwa ajili ya kusafisha nyasi, kukata na nyenzo nyingine huru, na kuruhusu kuondoa kwa urahisi kuunda ulaini, usawa wa udongo wakati wa kuondoa magugu zisizohitajika.
  5. Glovu za bustanini: Sio lazima lakini husaidia kuzuia malengelenge na mikwaruzo bila kusahau kuweka mikono yako safi.
  6. Kinyunyizio: Unaweza kumwagilia bustani yako ya mboga kwa bomba na kiambatisho cha kunyunyuzia, lakini kinyunyizio kitatumika kwa nafasi kubwa zaidi. Ikiwa unahitaji kumwagilia eneo kubwa.
  7. Toroli: Tumia kukusaidia kusongesha kiasi kikubwa cha udongo, mboji na mimea n.k.
Mboga zinastawi kulingana na msimu, hivyo ni vyema kufahamu aina ya mbogamboga zinazostawi katika msimu huo. Chagua mboga ambazo hazihitaji matunzo makubwa kwani hasara yake ni ndogo na zinazotoa mzao mzuri.Chagua nyingi na aina tofauti tofauti.  

Bustani ya jikoni, inaweza kuchukua mboga kama vile:

  1. Mboga za majani: Mchicha, mnavu, sukuma wiki, mgagani n,k
  2. Mazao ya mizizi: Karoti, vitunguu, radishi n.k
  3. Mikunde: Maharagwe, njegere, soya
  4. Mboga za matunda: Nyanya, ngogwe, pilipili kali/mbuzi, pilipili hoho

TEKNOLOJIA TOFAUTI ZA BUSTANI ZA JIKONI

BUSTANI ILIYOCHIMBWA MARA MBILI


BUSTANI YA KUNING’INIZA


BUSTANI TAIRI



BUSTANI DUARA/BUSTANI UPENDO


BUSTANI KIKAPU



BUSTANI MEZA


BUSTANI KICHUGUU

BUSTANI SANDUKU