
Katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabiachi zinazolikumba eneo la Tarime, Kituo cha Kilimo Mogabiri (MFEC) kimeendelea kuwa mwanga wa matumaini kwa jamii za wakulima. Kupitia mafunzo ya kilimo hai, matumizi ya mbegu za asili, uhifadhi wa maji, upandaji miti, na matumizi ya taarifa za hali ya hewa, kituo hiki kimeongeza uwezo wa wakulima wa vijiji kama Kitenga, Nkerege, Kwisarara na Turugeti kufanya maamuzi sahihi ya shughuli za kilimo na kuongeza uzalishaji ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Mbali na hilo, MFEC imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii kujiongezea kipato kupitia miradi ya lishe mashuleni, uanzishwaji wa vikundi vya akiba na mikopo (VICOBA), na uhamasishaji wa matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira. Kwa ushirikiano wa karibu na SAT kupitia uwezeshwaji wa matumizi ya zana shirikishi ya PACDR, kituo hiki kimeweza kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu wa Tarime – kiuchumi,kijamii na kimazingira. Jarida hili la habaro linakuletea baadhi ya mafanikio hayo, simulizi halisi na sauti za wanufaika walioguswa moja kwa moja na kazi hii muhimu .
SOMA ZAIDI